1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Clinton nchini Thailand

22 Julai 2009

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amewasili katika mkutano muhimu nchini Thailand akiwa na ujumbe kuwa Marekani iko tayati kushirikiana na bara la Asia.

https://p.dw.com/p/Iv7Y
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton.Picha: AP

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton alianza mazungumuzo na nchi za Asia katika mkutano wa kimataifa wa siku mbili katika kisiwa cha Phuket kujadili masuala yakiwemo ya Korea Kaskazini na Myanmar yakiwemo pia masuala mengine katika eneo hilo.

Clinton alisema kuwa, akiwa katika mji wa Phuket atatia sahihi makubaliano ya kuwepo ushirikiano wa nchi za Asia kusini ambayo yanatoa mwelekeo ya kutatua mizozo kwa njia ya amani, makubaliano amabayo tayari yametiwa sahihi na mataifa kumi yaliyo nje ya muungano huo wa ASEAN.

Clinton pia ameelezea vile Marekani itakabiliana na Iran kwa kuzihami nchi washirika wake na pia kuongeza makombora ya kujihami katika eneo hilo.Alisema kuwa kuendelea na mipango ya nuklia hakuwezi kuifanya Iran kuwa salama nchi ambayo Marekani inasema kuwa inaunda silaha za kinyuklia.

Tutaacha milango wazi wa mazungumzo na Iran lakini pia tumezungumza wazi kuwa tutachukua hatuakama vile nimekuwa nikisema mara kwa mara , hatua kali za kuimarisha usalama wa washirika wetu katika eneo hili, alisema Clinton akiwa mjini Bangkok.

Wiki iliyopia Clinton alisema kuwa nia ya Iran haijulikani kufuatia uchaguzi wa mwezi Juni na kuwa mazungumzo katik ya Mareknai na Iran kuhusu mipango yake ya nuklia bado yapo.Utawala uliopita wa rais George Bush ulikataa kufanya mazungumzo na Iran ukisema kuwa ni lazima uwe umetimiza masharti fulani lilkiwemo suala la kusitisha mipango ya nuklia.

Rais wa Marekani Barck Obama ambaye aliingia madarakani mwezi Januari anasema kuwa hata hivyo hatua hizo zilishindwa huku naye Clinton akizitaja hatua hizo kama makosa.

Hata hivyo Iran haijatoa jibu lolote kuhusu mbinu mpya za rais Obama na zile kutoka nchi zingine zinazolenga kuishinikiza Iran kusitisha mipango ya nuklia ambayo nchi za magharibi zinaamini kuwa ni yaakunda bomu la kinyukilia madai amabyo Iran inayakanusha na kusema kuwa mipango yake ni ya kuzalisha nishati.

Wakati huo huo Clinton hapo awali alisema kuwa uhusiano wowote wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Myanmar huenda ukahatarisha usalama wa nchi majirani wa Myanmar kusini mwa bara Asia. Clinton alisema kuwa kuwepo kwa usalamna katika eneo hilo ni lazima Korea isitishe mipango yake ya kinyukilia

Clinton alisema kuwa Marekani inafahamu mipango ya ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Myanmar, suala ambalo alisema ku,wa wanalichukulia k,wa undani, akiongeza kuwa hali hii inaweza kulivuruga eneo hilo na kuhatarishga usalama wa mataifa jirani wa Burma.

Korea Kaskazini ililifanyia jaribio kombora la kinyuklia mwezi Mei mwaka huu na makombora ya mengine saba ya masafa marefu mapema mwezi huu na kwenda kinyume na azimio la umoja wa mataifa.

Meli ya Korea Kaskazini ambayo ilidaiwa kubebya silaha zilizo pigwa marufuku mwezi Juni mwaka huu ilisemakana kelekea Myanmar lakini hata hivyo haikutia nanga katika bandari hiyo.

Mwandishi :Jason Nyakundi/RTRE

Mhariri :Othman Miraji