1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaJapan

China yasema iko tayari kuisaidia Japan baada ya tetemeko

3 Januari 2024

China imesema iko tayari kutoa msaada muhimu kwa Japan kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoipiga nchi hiyo siku ya Jumatatu na ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu 62.

https://p.dw.com/p/4aoz4
Athari za tetemeko la ardhi lililoipiga Japan
Athari za tetemeko la ardhi lililoipiga JapanPicha: Kyodo/REUTERS

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Wang Wenbin ameuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba hakujaripotiwa raia yeyote wa China aliyejeruhiwa katika tetemeko hilo ambalo ni baya zaidi kutokea nchini Japan tangu mwaka 2016.

Na katika tukio jingine huko Japan, mamlaka ya usafiri imeanzisha uchunguzi kufuatia ajali ya ndege ya abiria iliyogongana na ndege ya walinzi wa pwani na kusababisha vifo vya watu watano.

Ajali hiyo ilitokea kwenye uwanja wa ndege wa Haneda katika mji mkuu wa Japan, Tokyo.