1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yapinga vikwazo dhidi ya Iran

5 Februari 2012

Kansela Angela Merkel anaendelea na ziara yake nchini China ambako anatarajiwa kukutana na Rais Hu Jintao baada ya kukutana na Waziri Mkuu Wen Jiabao aliyemwambia kuwa China ina imani na sarafu Euro.

https://p.dw.com/p/13w9P
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa China Hu Jintao
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa China Hu JintaoPicha: dapd

Hapo jana Kansela Merkel alikutana na Waziri Mkuu Wen Jiabao aliemhakikishia Kansela huyo kuwa China itaendelea kuwa na imani na sarafu ya Euro. Waziri Mkuu Wen pia aliashiria utayarifu wa nchi yake katika kusaidia juhudi za kuutatua mgogoro wa madeni barani Ulaya.

Katika hotuba yake Kansela Merkel aliihakikishia China kwamba barala la Ulaya lipo imara kifedha kufuatia makubaliano juu ya kuzitekeleza taratibu za kuyadhibiti matumizi ya serikali. Kansela wa Ujerumani pia ameitaka China isaidie katika kuishawishi Iran iachane na mpango wake unaoweza kuwa wa kutengeneza silaha za nyuklia.

Hata hivyo gazeti kuu la chama cha kikomunisti cha China kimeshutumu vikwazo dhidi ya Iran wakati Kansela Merkel alipokuwa anakutana na Rais Hu Jintao hapo jana na baada ya kuitaka China iibane Iran ili iachane na mpango wa kuunda silaha ya nyuklia. Gazeti hilo la "Peoples Daily" limesema vikwazo dhidi ya Iran vitauathiri uchumi wa dunia.Katika maoni yake gazeti hilo limezitaka serikali za dunia ziwe makini na ziwe na subira badala ya kuivukuta mivutano.

Mwandishi: Abdu Mtullya/DPA
Mhariri: Mohammed Abdulrahman