1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

China na Urusi zamkingia kifua Assad

Mvutano wa wiki nzima wa kidiplomasia katika kupata msimamo wa pamoja katika umoja wa mataifa kuhusu Syria hauonyeshi kupata mafanikio.

Members of the United Nations Security Council listen to Syria's U.N. Ambassador Bashar Ja'afari during a Security Council meeting on the situation in Syria at United Nations headquarters Thursday, July 19, 2012. Russia and China vetoed a U.N. resolution to imposes non-military sanctions on Syria. (AP Photo/Kathy Willens)

Kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa

Wakati katika mji mkuu Damascus machafuko yanazidi kuongezeka, Urusi na China Alhamis (19.07) zilitumia kura zao za veto dhidi ya azimio la umoja huo dhidi ya Syria. Hii ni mara ya tatu nchi hizo kutumia kura zao za veto. Azimio hilo lilikuwa na lengo la kuweka vikwazo dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Assad.

Wakati rais wa baraza hilo Nestor Osorio kutoka Columbia alipowataka wanachama 15 wa baraza hilo kupiga kura kuhusu mswada wa azimio hilo, macho yote yaliwageukia wawakilishi wa Urusi na China. Na kama ilivyotarajiwa mikono yao ilikuwa tayari juu, ikiwa ni ishara ya upinzani wao.

A handout photo distributed by Syrian News Agency (SANA) on July 3, 2012, shows Syria's President Bashar al-Assad during an interview with a Turkish newspaper in Damascus. Assad has told a Turkish newspaper he wished his forces had not shot down a Turkish jet last month and that he would not allow tensions between the neighbouring countries to turn into open combat. It was not immediately clear when the interview was conducted. REUTERS/SANA/Handout (SYRIA - Tags: CONFLICT POLITICS) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS

Rais wa Syria Assad Syrien

China na Urusi zakinga kifua

Hii ni mara ya tatu, ambapo inazuwia hatua kali dhidi ya utawala wa Bashar al-Assad kwa kutumia kura zao za veto katika umoja wa mataifa. Balozi wa Uingereza katika umoja wa mataifa, Lyall Grant, amesema kuwa amesitushwa na uamuzi huo.

"Athari za matendo yao ni kuunga mkono utawala wa kikatili na wanaweka maslahi ya nchi zao mbele kuliko maisha ya mamilioni ya Wasyria."

Mwanadiplomasia huyo ambaye amekasirishwa na hatua hiyo amesema kuwa zaidi ya watu 14,000 wasio na hatia nchini Syria wameuwawa, tangu pale Urusi na China mwezi wa Oktoba mwaka jana zilipotumia kwa mara ya kwanza kura zao za veto kuukingia kifua utawala wa Assad. Mswada huo wa azimio ambao pia uliungwa mkono na Ujerumani, ambapo Pakistan na Afrika Kusini hazikupiga kura, ulipata kura 11 ambazo zingetosha kuupitisha kwa kura nyingi, ulikuwa unatishia kuuwekea vikwazo zaidi utawala wa Syria, iwapo utawala huo utaendelea kupinga mpango wa amani wa mjumbe wa kimataifa na wa jumuiya ya nchi za kiarabu kwa mzozo wa Syria, Kofi Annan.

U.N. Syria peace envoy Kofi Annan speaks to the media at a hotel after returning from a meeting with Syrian President Bashar al-Assad in Damascus July 9, 2012. REUTERS/Khaled al-Hariri (SYRIA - Tags: POLITICS)

Mjumbe wa kimataifa kuhusu Syria Kofi Annan

Muda wa ujumbe kuongezwa

Pamoja na hayo kutokana na hali ya kuongezeka kwa ghasia nchini Syria, kundi la uangalizi la umoja wa mataifa linapaswa kuongezewa muda wa kukaa huko kwa siku 45. Azimio la aina hii ni kwa maslahi ya mataifa ya magharibi na kwamba ni kisingizio cha kutaka kuhalalisha mashambulio ya kijeshi, amesema balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa, Vitaly Churkin.

"Vita vya mataifa mengine vinafanyika katika ardhi ya Syria, ambavyo havina uhusiano wowote na maslahi ya watu wa Syria."

NEW YORK, June 10, 2009 (Xinhua) -- U.S. UN Ambassador Susan Rice speaks to the media at the UN headquarters in New York, the United States, June 10, 2009. The five permanent members of the UN Security Council and Japan and South Korea on Wednesday reached agreement on a draft resolution in response to the nuclear test conducted by the Democratic People's Republic of Korea (DPRK), a diplomat said. Xinhua /Landov

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice

Maelezo ya balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa, Susan Rice, yameonyesha kuwa upinzani huo ni kama wenda wazimu. Urusi imekuja na mswada wa azimio lake ambalo linataka kurefushwa kwa ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Syria. Pakistan ikiungwa mkono na Urusi, inapendekeza kurefushwa kwa muda wa ujumbe huo wa umoja wa mataifa kwa siku 45. Uingereza inapendekeza kurefushwa huko kwa siku 30. Muda wa ujumbe huo umemalizika usiku wa manane leo Ijumaa. Kura inatarajiwa kupigwa leo.

Wakati huo huo, waasi nchini Syria wamedai kuwa wameviteka vivuko vya mpakani vya Syria kuingia Iraq na Uturuki. Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Iraq amesema wapiganaji wa jeshi la waasi la Syria huru wanadhibiti vivuko vyote katika mpaka wa nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa Iraq imeufunga mpaka wake kufuatia ulipizaji kisasi wa waasi dhidi ya majeshi ya Syria.

Mwandishi : Schmidt, Thomas / ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com