1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abdul Rahman Baba ajiunga na Chelsea kutoka Augsburg

17 Agosti 2015

Chelsea imemsaini beki wa kushoto Abdul Rahman Baba kutoka klabu ya FC Augsburg ya Ujerumani. Chelsea na Augsburg zimethibitisha kukamilisha usajili wa beki huyo raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 21 kupitia tovuti zao

https://p.dw.com/p/1GGkg
Fußball Abdul Baba beim FC Augsburg
Picha: picture alliance/Eibner-Pressefoto

Usajili huo umefanyika kujaza nafasi ya beki wa kushoto baada ya Mbrazil Luis Filipe kurudi katika timu yake ya zamani ya Atletico Madrid nchini Uhispania

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho, amepongeza usajili huo akisema kuwa anaamini mlinzi huyo ataleta ushindani kwa Cesar Azpilicueta katika nafasi ya beki wa kushoto.

Rahman amekuwa katika klabu ya Augsburg kwa miezi 12 ambako alisajiliwa akitokea timu ya SpVgg Greuther Fürth mnamo Agosti mwaka 2014.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Sessanga