1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHARLESTONE:Wagombea urais Marekani katika mdahalo wa kihistoria

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfr

Wagombea Urais kupitia chama cha Democratic nchini Marekani kwa mara ya kwanza historia ya siasa duniani wamefanya mdahalo kupita mtandao wa internet ambapo wapiga kura nchini humo waliwauliza maswali moja mwa moja.

Zaidi ya watu elfu 3 walituma maswali yao kwa kutumia teknolojia hiyo iitwayo YouTube ambapo wagombea waliyajibu moja kwa moja katika mdahalo uliyomalizika muda mfupi uliyopita.

Seneta Barak Obama wa jimbo la Illinois ambaye baba yake ni Mkenya anachuana na Seneta wa New York Hillary Clinton ambaye ni mke war ais wa zamani Bill Clinton kuwania kuteuliwa na chama hicho kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

Uchaguzi wa chama hicho cha Democratic kumpata mgombea wake unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba.

Katika Mdahalo huo, Maswali juu ya Vita nchini Irak, mabadiliko ya hali ya hewa duniani na mzozo wa Darfur yaliulizwa kwa wagombea, ambapo Barak Obama, Hillary Clinton na Seneta Edward Kennedy waliwasisimua wengi.