Champions League | Michezo | DW | 29.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Champions League

Weder Bremen yaitandika Real Madrid 3-2 katika champions League

default

Schalke (buluu)

Mabingwa wa kombe la ulaya la klabu bingwa -Ac Milan ya Itali na Chelsea ya Uingereza, ndizo zilizoondoka jana uwanjani na tiketi zao za kucheza duru ijayo ya kutoana ya champions League.Licha ya pigo la jana huko Bremen, Real Madrid,mabingwa mara kadhaa wa ulaya wanaweaza kuingia duru ijayo.Werder Bremen ya Ujerumani, ilitamba jana mbele ya Real Madrid ya Spain ilipoichapa mabao 3-2 na kufufua matumaini yao ya kucheza duru ijayo mradi tu watambe mbele ya Olympiakos ya Ugiriki, mwezi ujao.

Licha ya pigo la jana la mabao 3-2 huko Bremen,Real Mdrid bado wana nafasi nzuri ya kujiunga na AC Milan,mabingwa na Chelsea zilizokata jana tiketi zao za duru ijayo ya kutoana.Kwani, Real wako pointi sawa sasa na Olympiakos ya Ugiriki walioilaza jana Lazio mjini Roma.

Bremedn kibarua chake kijacho kitakua huko Ugiriki nyumbani mwa Olympiakos na kama Lazio Roma, wana pointi 6 sasa .Roma laklini watabidi kuitembelea Real nyumbani mwao mjini Madrid.

Kusema kweli,Real ambao hawakuweza kucheza na staid wao Diego aliefungiwa,hawana rekodi nzuri Ujerumani.Katika mapambano 22,Real imewika mara 1 tu Ujerumani.

Breemn ilianza uzuri jana pale Markus Rosenberg,alipolifumania lango la Real tayari mnamo dakika ya 4 ya mchezo.Dakika 9 baadae, Robinho, alitoa jibu la Real akidai “kutangulia si kufika.”Lakini, alikuwa tena Rosenberg alietikisa ngome ya Real. Muivory Coast Boubacar Sanogo,akaipatia Bremen bao la pili –shukurani kwa pasi maridadi kutoka Rosenberg.Aaaron Hunt akaupiga msumari 3 katika jeneza la Real usiku wa jana kabla Van Niestelroy, kupunguza mwanya kwa bao la pili la Real mnamo dakika ya 53 ya mchezo.

Bao hilo lakini, halikutosha kuinusuru Real,kuzikwa katika kaburi waliochimbiwa na Rosenberg usiku wa jana.

Valencia –kalbu nyengine ya Spain, ikicheza na wachezaji 10 tu ,haikumudu zaidi ya suluhu 0:0 na Schalke-klabu nyengine ya Ujerumani.Sasa Schalke imefufuka na inaweza kuingia duru ijayo ikiwa tu itatamba mbele ya Rosenborg Trondheim, iliochezeshwa kindumbwe-ndumbwe nyumbani na kuzabwa mabao 4:0 na Chelsea.

Mabao 2 ya Didier Drogba na 2 mengine kutoka Alex na Joe Cole yameipeperusha jana Chelsea katika duru ijayo ya timu 16 za champions League.

Liverpool nayo imetamba kwa mabao 4-1 dhidi ya Porto ya Ureno. Hii ina maana, Liverpool itahitaji sasa ushindi katika changamoto ijayo na Olympique Marseille ya Ufaransa kuingia duru ijayo.

 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUVF
 • Tarehe 29.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CUVF