1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Chama kipya cha TNA chazinduliwa Kenya

Naibu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua chama chake kinachoitwa TNA The National Alliance hapo jana huku akisisitiza tena azma yake ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.

Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Uhuru ambaye anatakiwa na mahakama ya jinai ya ICC kwa tuhuma za kupanga ghasia za baada ya uchaguzi nchini humo mwaka wa 2007/2008 amesema chama chake kitafanya kazi na vyama vingine vya kiasiasa nchini humo vyenye nia njema na taifa hilo.

Amina Abubakar amezungumza na mchambuzi wa maswala ya kisiasa nchini Kenya Martin Oloo kuhusu swala hili la uzinduzi wa TNA akitaka kufahamu sura halisi ya mambo yalivyo baada ya kuundwa chama hicho.

(Kusikiliza mahojiano bonyeza alama ya spika ya masikioni)

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Yusuf Saumu

Sauti na Vidio Kuhusu Mada