1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Putin chapata ushindi.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CW4I

Moscow. Vyama vitatu vinavyounga mkono serikali kwa pamoja vimepata asilimia 80 ya kura katika uchaguzi wa jana Jumapili nchini Urusi. Chama cha rais Vladimir Putin cha United Russia pekee kimepata asilimia 64.

Wachunguzi wanatarajia kuwa matokeo hayo yatampatia kiongozi huyo ushawishi mkubwa na kuendeleza udhibiti wake hata baada ya kujiuzulu kutoka wadhifa wa urais mwakani kama anavyotakiwa na katiba ya nchi hiyo. Vyama vya upinzani vinaishutumu serikali kwa kupanga matokeo na kwa kutumia mbinu za kuwabana wapinzani.

Chama cha Kikomunist , ambacho kimepata asilimia 11 ya kura , kimesema kuwa huu ulikuwa uchaguzi mbaya kabisa katika wakati baada ya utawala wa Urusi ya zamani na kimeapa kupinga matokeo hayo. Marekani pia imetaka kufanyike uchunguzi kuhusiana na mapungufu kadha katika uchaguzi huo.