Chama cha Kansela Merkel chashindwa katika mikoa miwili
31 Agosti 2009Katika mkoa wa magharibi mwa Ujerumani wa Saarland na Thuringia uliyoko katika iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki chama hicho cha CDU kimepata asilimia 34.5 na 32.5 ya kura.
Muungano wa vyama vitatu vya Social Democrats SPD,kile cha mrengo wa shoto cha “Linke” pamoja na kile cha walinzi wa mazingira, unaonekana dhahiri kushinda katika mkoa wa Saarland.
Katika mkoa wa Thuringia bado haijawa wazi iwapo chama cha Social Democrats ambacho kimepata kura chache kuliko kile cha Linke, kimekubali kuingia katika muungano na vyama vingine kikiwa na sauti ndogo.
Katika mkoa wa mashariki wa Saxony chama cha Kansela Merkel kimepata asilimia 41 ya kura kiwango ambacho ni sawa na kile ilichopata katika uchaguzi uliyopita.Chama kinachounga mkono wafanyabishara cha Free Democrats, FDP kimepata asilimia kumi ya kura ikiwa ni onagezeko la asilimia 4.
Waziri Mkuu wa mkoa huo wa Saxony Stanislaw Tillich kutocha chama cha CDU Stanislaw Tillich aliwashukuru wananchi kwa kukipa tena ushindi chama chake.
Baadhi ya wadadisi wanaona matokeo katika mikoa hiyo, ni mtihani muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa Ujerumani Septemba 27 mwaka huu.
Kansela Merkel anategemea kuunda muungano na chama cha FDP, baada ya chaguzi zote hizo, ili kuweza kuweka mabadiliko katika mfumo wa kodi na sera nyinginezo.
Mwandishi:Aboubakary Liongo