Castro kuton’gan’gania madaraka milele
18 Desemba 2007Matangazo
HAVANA
Kiongozi alie mgonjwa wa Cuba Fidel Castro ambaye hakuonekana hadharani kwa miezi 16 amedokeza hapo jana kwamba yumkini akaacha nyadhifa zake rasmi.
Castro mwenye umri wa miaka 80 amesema kwenye baruwa iliosomwa katika televisheni kwamba wajibu wake wa msingi sio kun’gan’gania nyadhifa na kuwa kikwazo kwa vijana kuingia madarakani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Castro kuzungumzia juu ya uwezakano wa kustaafu.