Casablanca, Morocco. Mtu mmoja ajilipua. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Casablanca, Morocco. Mtu mmoja ajilipua.

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga nchini Morocco , amelipua milipuko katika dula watu wanapopata huduma za mtandao wa Internet, na kujiua mwenyewe na kuwajeruhi wengine wanne.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa mtoto wa mwenye duka hilo aliingia katika mabishano na mtu huyo wakati bomu lililofichwa katika nguo zake lilipolipuka.

Bomu hilo linaaminiwa kuwa lililipuka kwa bahati mbaya.

Polisi wamesema kuwa mtu huyo aliyejilipua , alikuwa anapanga shambulio katika eneo ambalo halikufahamika , na aliingia katika duka hilo kupata maelekezo ya mwisho kupitia barua pepe. Tukio hilo lilitokea katika kitongoji cha Sidi Moumen , mjini Casablanca ambako bomu la kujitoa muhanga liliuwa watu 45 mwaka 2003.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com