1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARACAS:Makampuni ya Kimarekani yamgomea Charvez

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnt

Makampuni mawili makubwa ya mafuta ya Kimarekani, yamekataa nafasi iliyotolewa na Rais Hugo Charvez wa Venezuela kuendela kufanyakazi nchini humo kwa masharti.

Rais Charvez alitangaza kutaifisha sehemu kubwa ya hisa katika sekta ya mafuta na jana ilikuwa siku ya mwisho kwa makampuni kukubali ama kuondoka.

Hata hivyo makampuni mengine kutoka Marekani, Uingereza, Norway na Ufaransa zimekubaliana na uamuzi huo wa Charvez na kutia saini makubaliano ya kuendelea na kazi hiyo.