CARACAS:Castro asikika kwenye kipindi cha mojakwa moja Redioni
28 Februari 2007Matangazo
Rais wa Cuba Fidel Castro amesema anaendelea kupata nafuu na kujisikia mwenye nguvu baada ya kuugua maradhi ya tumbo.
Castro aliyasema hayo akizungumza moja kwa moja katika kipindi cha redio pamoja na mshirika wake rais wa Venezuela Hugo Chavez.
Tukio hilo limewashtukiza wasikilizaji ambao hawakutarajia kumsikia kwa sasa kiongozi huyo kutokana na hali yake ya kiafya.