1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CARACAS: Stesheni ya RCTV yafungwa Venezuela

Nchini Venezeuela,maelfu ya watu walioandamana mji mkuu Caracas,kupinga kuifungwa kwa stesheni ya televisheni RCTV,wamefyatuliwa risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi.Maandamano yalifanywa katika miji mbali mbali nchini humo,baada ya Rais Hugo Chavez kutoa amri ya kuifunga stesheni ya RCTV kuanzia usiku wa manane wa siku ya Jumapili. Hugos,ameilaumu stesheni hiyo kuwa ilichochea harakati za kisiasa.Sasa,serikali ya Venezuela imeishtaki stesheni nyingine ya televisheni Globovision kuwa ilihimiza kumuuawa rais Chavez. Mkurugenzi wa stesheni hiyo,Alberto Ravel alipozungumza mjini Caracas alisema,chombo hicho cha habari hakitotishwa na wala hakitokubali kushinikizwa na serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com