CAPE TOWN: Mbeki atumaini chaguzi huru Zimbabwe | Habari za Ulimwengu | DW | 31.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAPE TOWN: Mbeki atumaini chaguzi huru Zimbabwe

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini anaamini kuwa uchaguzi mkuu utakaofanywa mwakani nchini Zimbabwe utakuwa huru na wa haki,licha ya kuhofiwa kinyume na hivyo.Akijibu masuala bungeni,Mbeki alisema,amehakikishiwa na serikali ya Zimbabwe,jamii za kiraia na mashirika yasio ya kiserikali kuwa wataweza kukubaliana taratibu za kuhakikisha kuwa uchaguzi utakuwa wa haki.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alie na miaka 83 anaiongoza Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1980 na anatazamiwa kugombea urais katika chaguzi za rais na bunge zitakazofanywa mwezi wa Machi.Chaguzi kuu mbili za mwisho ziligubikwa na madai ya vitisho na udanganyifu wa kura.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com