CANBERA: Howard aahidi msaada zaidi kwa Irak
19 Februari 2007Matangazo
Waziri mkuu wa Australia, John Howard, amesema nchi yake huenda ikaongeza msaada wake nchini Irak. Hata hivyo, Howard hakusema ikiwa atapeleka wanajeshi zaidi kwenda Irak.
Idadi ya wanajeshi nchini Irak na Afghanistan inatarajiwa kuwa mada muhimu wakati wa mazungumzo yake na makamu wa rais wa Marekani, Dick Cheney, atakayeitembelea Australia wiki hii.
Howard amesema walimu wa jeshi zaidi huenda wakapelekwa Irak, ambako wanajeshi 1,400 wa Ausatralia wanahudumu.