Cameron aahidi kuwasaka waliofanya ghasia
12 Agosti 2011Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi jana kuwasaka wale waliohusika na ghasia, uporaji wa mali na uchomaji moto majumba na magari, hali iliyotokea wiki iliyopita katika miji kadha nchini Uingereza.
Akizungumza bungeni, Cameron ameelezea mipango ya kuzuwia ghasia kama hizo kutokea tena hapo baadaye, ikiwa ni pamoja na kutoa mamlaka kwa polisi, kuliita jeshi kusaidia, na pengine hata kuweka hali ya kutotembea usiku. Mamia ya watuhumiwa wa uporaji kwa sasa wamefikishwa katika mahakama za Uingereza baada ya siku nne za ghasia za usiku. Utulivu umerejea katika miji mikubwa ya nchi hiyo na polisi 16,000 wataendelea kuwapo katika mitaa ya mjini London hadi mwishoni mwa juma