1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CALIFORNIA:Moto mkubwa unaendelea kuwaka

Moto mkubwa unaendelea kuwaka katika jimbo la California nchini Marekani.

Takriban wakaazi milioni moja wamelazimika kuyahama makaazi yao kuukimbia moto huo mkubwa.

Karibu nyumba elfu moja na mia nane zikiwemo nyumba za biashara zimeharibiwa na moto huo katika eneo la pwani la kusini.

Afisa mmoja wa wazima moto katika eneo lililoathirika zaidi la San Diego amesema mkasa huo wa moto ni mbaya zaidi ambao kuwahi kutokea.

Rais George W. Bush ametangaza hali ya dharura katika wilaya saba za jimbo la California na taarifa ya ikulu ya Marekani imesema kuwa rais Bush atazuru jimbo la California kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com