CAIRO: Kivuko kimezama katika mto Nile
18 Agosti 2007Matangazo
Kivuko kilichopakia watu mia kadhaa waliokuwa wakisherehekea harusi,kimezama katika Mto Nile nchini Misri.Kwa mujibu wa polisi,watu wapatao darzeni kadhaa hawajulikani walipo.Feri hiyo ilitia nanga nje ya mji wa Beni Suef na iliinamia upande mmoja,wageni walipokuwa wakiimba na kucheza.