1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO : al Maliki aamuru kusitisha ujenzi wa ukuta Baghdad

23 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7p

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki ameamuru kusitishwa kwa ujenzi wa ukuta tata katika mji mkuu wa Baghdad.

Jeshi la Marekani limesema ukuta huo wa saruji kwenye wilaya ya Adhamia ulikuwa umekusudiwa kuitenganisha sehemu inayokaliwa na Wasunni wengi dhidi ya maeneo ya Washia kama hatua ya usalama.Maliki ambaye yuko mjini Cairo Misri katika ziara ya mataifa manne ya Kiarabu amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali yake itatafuta hatua mbadala za kulinda eneo hilo la Wasunni ambapo wakaazi wamesema ukuta huo utawatenganisha na jamii nyengine pamoja na kuzidisha mfarakano wa madhehebu.

Waasi wameimarisha mashambulizi yao mjini Baghdad ambapo hapo jana watu 18 wameuwawa na wengine 90 kujeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha kwenye kituo cha polisi mjini Baghdad na watu wenye silaha wamewauwa watu 23 wa kabila la watu wachache la Yazidi katika mji wa kaskazini wa Mosul.