Bush afanikiwa Saudi Arabia | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.01.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Bush afanikiwa Saudi Arabia

Rais George Bush wa Marekani leo ameendelea na ziara yake ya siku mbili nchini Saudi Arabia, ambapo amejadili masuala kadhaa na mfalme Abdullah wa nchi hiyo.

default

Rais Bush na Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia

Rais Bush amefanikiwa kuifanya Saudi Arabia ifikirie juu ya kuongeza uzalishaji wa mafuta. Hatua hiyo inatokana na mazungumzo aliyofanya na wenyeji wake ambapo amelalamika kuwa uchumi wa nchi yake unaathirika kutokana na bei ya juu ya mafuta.

Katika ziara yake nchini Saudi Arabia rais Bush pia amezungumzia suala la mashariki ya kati na ameitaka Saudi Arabia iunge mkono mchakato wa mazungumzo na maridhiano unaohimizwa na Marekani.

George Bush pia amezungumzia juu ya anachoita hatari kutoka Iran na kusema nchi yake itasimama pamoja na rafiki zake katika kuikabbili hatari hiyo.

Amesema Iran ni mfadhili mkuu wa ugaidi duniani kote na kwamba matendo yake yanahatarisha usalama wa mataifa yote.

Katika hatua za kukabiliana na hatari hiyo rais Bush amesema atasonga mbele na mradi wa silaha baina ya nchi yake na Saudi Arabia.

Amelifahamisha bunge la nchi yake juu ya mpango wa kuiuzia Saudi Arabia silaha za kisasa thamani dola milioni 120.

Rais Bush atamaliza ziara yake ya mashariki ya kati kwa kuitembelea Misri hapo kesho.

 • Tarehe 15.01.2008
 • Mwandishi Abdu Mtullya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Cq27
 • Tarehe 15.01.2008
 • Mwandishi Abdu Mtullya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Cq27

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com