1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Burkina yafukuza waandishí habari wa magazeti ya Ufaransa

2 Aprili 2023

Burkina Faso imewafukuza waandishí habari wa magazeti ya Ufaransa ya Le Monde na Liberation. Ni hatua ya karibuni kuchukuliwa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi dhidi ya vyombo vya habari vya Ufaransa

https://p.dw.com/p/4PbW5
Burkina Faso Ouagadougou | Journalisten
Picha: Zoeringer/Imagespic Agency/IMAGO

Burkina Faso imewafukuza nchini waandishí habari wa magazeti ya Ufaransa ya Le Monde na Liberation. Ni hatua ya karibuni kuchukuliwa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi dhidi ya vyombo vya habari vya Ufaransa.

Gazeti la Le Monde limesema mwandishi wao a Burkina Faso Sophie Douce ametimuliwa nchini humo pamoja na mwenzake wa Liberation Agnes Faivre.

Gazeti hilo limeitaja hatua hiyo kuwa ni ya kiholela na isiyokubalika. Waandishi hao wawili waliwasili Paris mapema leo baada ya kufukuzwa jana usiku. Jumatatu wiki hii, watawala wa kijeshi Burkina Faso walisitisha matangazo yote ya televisheni ya France 24, baada ya kumhoji mkuu wa Al-Qaeda tawi la Afrika Kaskazini.