1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUR HAKABA: Mapiganao makali yazuka

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0X

Mapigano makali yamezuka mapema leo mjini Bur Hakaba katikati mwa Somalia, kati ya majeshi ya serikali ya wanamgambo wa kiislamu. Mji wa Bur Hakaba unapatikana kati ya mji mkuu Mogadishu na mji wa Baidoa, ambao ni makao makuu ya serikali ya mpito ya Somalia.

Ethiopia inaiunga mkono serikali ya mpito ya Somalia inayokabiliwa na kitisho cha wanamgambo wa kiislamu waliouteka mji mkuu Mogadishu mnamo mwezi Juni mwaka huu na wanaoyadhibiti maeneo mengi ya kusini na katikati mwa Somalia.

Wanamgambo wa kiislamu wameanzisha utawala wa sharia katika maeneo wanayoyadhibiti na wametangaza vita vitakatifu vya jihad dhidi ya Ethiopia.