1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge lamuunga mkono Mizengo Pinda

9 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D4tt

Dar-es-salaam:

Bunge la Tanzania limeridhia kuteuliwa bwana Mizengo Pinda kuwa waziri mkuu mpya,baada ya bwana Edward Lowassa kuamua kujiuzulu.Wabunge 282 wamempigia kura na 279 wamempinga.Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 59 anakabidhiwa wadhifa wake hii leo bungeni mjini Dodoma.Duru za kuaminika zinasema huenda baraza jipya la mawaziri likatangazwa jumatatu ijayo.Waziri mkuu wa zamani,Edward Lowassa amejiuzulu kufuatia madai ya kuhusika na kashfa ya rushwa inayohusu kandarasi ya nishati na kampuni ya Marekani Richmond. Kisa hiki kimejiri wiki moja kabla ya ziara ya rais George W. Bush wa Marekani nchini Tanzania.