1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga

Ramadhan Ali14 Mei 2007

Bundesliga ikizidi kupambamoto,imegeuka mbio za farasi 2:Schalke 04 na Stuttgart iliony

https://p.dw.com/p/CHcC
Kuranyi akamata kichwa -Schalke yateleza.
Kuranyi akamata kichwa -Schalke yateleza.Picha: AP

Bundesliga imegeuka kitanmdawili,kwani timu 2 Schalke waliokua viongozi wa Ligi na Bremen-poimnti 2 nyuma, waliteleza na sasa Stuttgart imenyakua usukani huku mpambano 1 tu ukisalia kumtawaza bingwa-je, itakua timu gani-Stuttgart au Schalke ? Tutawachukua katika viwanja vya michezo huko Afrika Mashariki na kati-tukitupa macho jinsi Taifa Stars-timu ya taifa ya Tanzania inavyojiwinda kwa changamoto na Senegal na Ugandan cranes dhidi ya Nigeria kuania tiketi ya Ghana 2008.

Nitawachukua Kenya tukiitupia macho Ligi kuu,riadha na hata ringi ya mabondia na tutamalizia Kigali,Ruanda ambako majogoo wa riadha walikuwa barabarani kwa mbio za marathon.

Kinyan’ganyiro cha ubingwa wa Ujerumani hadi jumamosi kilikua kati ya timu 3-Schalke waliokua viongozi wa Ligi-Stuttgart waliokuwa pointi 1 nyuma na Bremen pointi 2 nyuma ya viongozi wa Ligi na kwamba kila moja kati ya timu hizo 3 ingeweza jumamosi ijayo kutoroka na kombe la ubingwa.

Baada ya firimbi ya mwisho kulia, Schalke walilazwa mabao 2:0 na mahasimu wao wa mtaani Borussia Dortmund .Bremen nayo ikalazwa nyumbani mabao 2:1 na Frankfurt.Ni Stuttgart tu kati ya timu hizo 3 iliothubutu kumpunga shetani wake na kutoroka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bochum.

Sasa kinyan’ganyiro cha ubingwa wa Bundesliga ni kati ya timu 2-Stuttgart wanaoongoza kwa pointi 2 dhidi ya Schalke.Hukumu itakatwa jumamosi ijayo.

Jogoo la Stuttgart, kutoka Brazil Cacau aliekwishatia mabao 13 msimu huu alisema baada ya changamoto hiyo:

“Ushindi wetu umetokana na kucheza kwa ari moja na timu moja,nguvu moja.hii imetuwezesha kugeuza mkondo wa mchezo.”-asema Cacau

Nae kocha wa Stuttgart Armin Veh,alisema:

“Tunataka kuwa mabingwa ,lakini si semi tutachukua ubingwa ,kwani wengi wamejitapa hivyo na halafu wakatoka mikono mitupu.ni siku ya mwisho ndipo hesabu itafanywa.”

Armin Veh, kocha wa stutgart inayoongoza sasa kwa pointi 2.

Tujiunge sasa na mwanamichezo wetu George Njogopa, akituarifu jinsi wadau wamedani ya dimba nchini Tanzania wanavyoutathmini uamuzi wa kocha wao kutokla Brazil kuijenga upya Taifa Stars kabla changamoto na Senegal juni 2.