Bundesliga msimu mpya kuanza | Michezo | DW | 03.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bundesliga msimu mpya kuanza

Ijumaa ijayo,firimbi italia kuanzisha msimu mpya wa Bundesliga.Nani wataibuka mabingwa ni vigumu kusema.Hatahivyo, Stuttgart mabingwa wa sasa wamepania kubakia na taji.

Kinyume na misimu iliopita ilivyoweza kubashiriwa FC Bayern Munich wangeibuka mabingwa mabingwa lakini hawakuibuka, msimu huu ni vigumu kubashiri.

“Na sasa mpira umekwisha.VFB Stuttgart ndio mabingwa wapya wa Ujerumani.”

Hivyo ndivyo mtangazaji alivyokuwa akisimulia siku ya mpambano wa mwisho wa msimu uliopita wa Bundesliga.

Kwa kweli, Stuttgart sio miongoni mwa timu zilizotazamiwa kutawazwa mabingwa msimu uliopita-ilikua ama Munich,Bremen au Schalke.

Kocha wa Stuttgart Armin Veh ndie aliewanoa chipukizi wake na kuwatundika kileleni mwa Bundesliga na ana yakini:

“ Tulistahimki kutawazwa mabingwa.”

Firimbi ikilia ijumaa ijayo,Stuttgart imeshaonya kwamba-mramba asali-harambi mara moja.Inataka kutwaa tena kombe hilo.Kinyume na B.Munich na klabu nyengine, mabingwa Stuttgart, hawakutumia sana kununua wachezaji wengi wapya kujiimarisha zaidi.

Kwahivyo, ukimuliza kocha wao Armin Veh aague ni timu gani itaibuka mabingwa:yeye anautupa mzigo huo mabegani kwa Bayern munich.

“Wakutazamiwa kuondoka na ubingwa ni bayern Munich nah ii ni wazi.”

Ikiwa fedha zanunua taji,basi kweli-Bayern Munich lazima tena ipigiwe upatu kuibuka mabingwa msimu ujao.wametumia kitita cha Euro milioni 70.

Wamemnunua Luca Toni,wa mabingwa wa dunia Itali.Wamemtia mfukoni Franck Ribery wa makamo-bingwa wa dunia-Ufaransa na wamemtorosha kutoka Bremen,mshambulizi wa Taifa Miroslav klose.

Hatahivyo, kati ya wiki hii,katika mpambano wa majaribio na FC cologne itakayocheza daraja ya pili msimu ujao,Munich ilizabwa mabao 3:1 mjini Cologne.

Kocha wa Bayern Munich Ottmar Hitzfeld,anahisi kwa kikosi alichonacho,timu yake imezidi kuvutia kwa mashabiki wake.

“Kutokana na wachezaji tuliowanunua,bila shaka ujerumani nzima imefurahia kuwa na wachezaji maarufu katika Bundesliga.hii inanufaisha kila timu.”

Zaidi lakini, itakua Bayern munich ikiwa itaweza kufuta madoa ya msimu uliopita ilipomaliza nafasi ya 4 katika ngazi ya ligi na kukosa hata tiketi ya kucheza msimu ujao katika champions League.

Hatahivyo, kocha wa B.Munich anaitazamia zaidi Schalke –makamo-bingwa kuipa changamoto kali zaidi hata kupita mabingwa Stuttgart:

“Schalke imebainisha wazi wazi kwamba sio timu ya kuidharau msimu mpya.”

Kwa kweli, Schalke wanataka kuvaa tena taji baada ya kupita kitambo cha miaka 50 tangu kulitwaa mara ya mwisho.Kocha wao Mirko Slomka amechishwa na Schalke kumaliza tu makamo-bingwa huku akiziona Bremen na munich na msimu uliopita Stuttgart wakitoroka na kombe.

Anasema:

“Sisi tuna nguvu na naamini tunaweza pia kuwapa changamoto Bayern Munich.”

Kuna klabu nyengine hazihanikizi wakati huu lakini zaweza kuzusha msangao na kutoka nyuma zikjatia for a usoni:Hamburg,Borussia Dortmund,Bayer Leverkusen na hata Wolfsburg chini ya kocha wake mpya Felix Magath alietimuliwa huko munich.

Katika daraja ya pili ya Bundesliga,changamoto msimu huu ujao ndio kali zaidi kwani klabu nygini za daraja ya kwanza za zamani zitatapia kuania nafasi 3 za kupanda tena daraja ya kwanza.

Tena kila moja imejiimarisha kwa wachezaji wapya-kama vile FC Cologne,Kaiserslauten na Munich 1860.

Katika daraja ya pili ni vigumu pia kubashiri ni timu gani 3 kweli zitapanda daraja ya kwanza-kila kitu chawezekana.

 • Tarehe 03.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbU
 • Tarehe 03.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHbU