1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUDAPEST: Kansela Merkel azuru Greenland

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYP

Kansela wa Ujerumani, Bi Angel Merkel, na waziri wa mazingira, Sigmar Gabriel, wamo nchini Greenland kwa ziara rasmi ya siku mbili.

Lengo la ziara hiyo ni kutathmini athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika kisiwa hicho. Viongozi hao wameandamana na wanasayansi mashuhuri wa Ujerumani kisiwani humo.

Kansela Merkela amesema, ´Nadhani kuwa hata sisi pia tuna nafasi zote tutakapofanya jambo la sawa kuhifadhi nishati, kupunguza utoaji wa gesi ya carbon dioxide na hivyo basi kuwa na nafasi nzuri ya kukabiliana na swala hilo. Na nafikiri Ulaya inatakiwa kuongoza katika teknolojia na uvumbuzi ili tutumie uwezo wetu kutengeza nafasi mpya za ajira na kuongeza usafirisahji wa bidhaa katika nchi za kigeni.´

Kansela Merkel alilipa kipaumbele tatizo la ongezeko la joto duniani kwenye ajenda ya mkutano wa nchi za G8 uliofanyika mjini Heiligendamm hapa Ujerumani miezi miwili iliyopita.

Wakati wa ziara yake nchini Greenland, kansela Merkel atatembelea maeneo mbalimbali kuona jinsi barafu inavyoyeyuka na kuanguka baharini.