1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels.Wanasiasa Ulaya wachoshwa na siasa ya nje ya Marekani.

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCu6

Wanasiasa wa Ulaya wamesema kuwa wanategemea Marekani itabadilisha mwenendo wa sera yake ya kigeni, kufuatia matokeo ya uchaguzi uliofanyika wiki hii nchini Humo.

Elmar Brok mwanasiasa wa Ujerumani katika Bunge la ulaya amesema, anategemea kuwa hii itakuwa ni nafasi nzuri kwa Washington kubadilisha sera zake nchini Iraq na Afghanistan.

Ameongeza kuwa, anamatumaini kwamba chama cha Democrats katika Baraza la Congress kitamshinikiza rais kukubali kuondoshwa kwa vikosi vya kijeshi vya Marekani nchini Iraq.

Mapema mkuu wa sera za nje wa umoja wa Ulaya, Javier Solana, amekuita kujiuzulu kwa Donald Rumsfeld kwamba Washngton sasa imebadilisha sera zake nchini Iraq.