1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Wakimbizi wa Somalia kupewa msaada zaidi

8 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtb

Umoja wa Ulaya unaidhinisha msaada wa dola milioni 4 mahsusi kwa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa raia wa Somalia walioachwa bila makao.Fedha hizo zitatumika kujenga makao,chakula,maji vilevile huduma za matibabu kwa waSomali wanaokimbia mapigano ya hivi karibuni kati ya wanamgambo wa kiislamu na majeshi ya Ethiopia yanayounga mkono majeshi ya serikali ya muda ya Somalia.

Kwa mujibu wa maafisa wa Umoja huo msaada zaidi unahitajika kufuatia ukame,mafuriko na mchipuko wa ugonjwa wa homa ya Riftvalley.Fedha hizo ni nyongeza ya zile zilizotolewa na Umoja wa Ulaya mwaka huu.Kamishna anayehusika na misaada ya kibinadamu katika Umoja huo Olli

Rehn anatoa wito kwa wapiganaji kushirikiana na serikali ili kusitisha vita.

Wakati huohuo mkutano wa maridhiano ya kitaifa unatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi Juni utakaoshirikisha vikundi vinavyopingana nchini Somalia.Nchi ya Somalia imekumbwa na ghasia tangu kungolewa madarakani kwa Siad Barre mwaka 91.

Umoja wa Ulaya umeshatoa euro milioni 32 u nusu za misaada ya kibinadamu kwa nchi ya Somalia tangu mwaka 2004.