1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Umoja wa Ulaya kuiongezea vikwazo Myanmar

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKQ

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakubali kuongeza vikwazo dhidi ya utawala wa Kijeshi wa Myanmar ili kupinga hatua ya uongozi huo ya kushambulia waandamanaji wanaodai demokrasia.Ureno iliyo mwenyekiti wa Umoja huo imetoa taarifa inayoiwekea serikali ya Myanmar vikwazo vya ziada vitakavyojumuisha usafiri wa wanajeshi vilevile bidhaa zinazouzwa nje mfano mbao na vito vya thamani.

Mapendekezo hayo mapya yanasubiri kuidhinishwa na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya katika kipindi cha majuma mawili yajayo.Umoja wa Ulaya tayari unaiwekea Myanmar vikwazo ila kusisitiza umuhimu wa mataifa jirani ya Uchina na India kuishinikiza.Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa Ibrahim Gambari bado anasubiriwa kutoa taarifa yake kuhusu ziara ya siku nne nchini humo.

Japan tayari imetangaza kusitisha msaada kwa Myanmar kufuatia kupigwa risasi hadi kufa kwa raia wake mmoja aliyekuwa mwandishi mjini Yangon.