BRUSSELS:NATO yalalamika juu ya hatua ya Urusi kujitoa kwenye mkataba | Habari za Ulimwengu | DW | 15.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS:NATO yalalamika juu ya hatua ya Urusi kujitoa kwenye mkataba

Nchi za mfungamano wa kijeshi wa NATO zimeeleza wasi wasi juu ya hatua ya Urusi kusimamisha utekelezaji wa mkataba juu ya kudhibiti silaha za kawaida barani Ulaya.

Rais Vladimir Putin wa Urusi ametia saini agizo juu ya hatua hiyo itakayoanza kutekelezwa na Urusi baada ya siku 150 kwa mujibu wa mkataba huo.

Hatahivyo naibu waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Gernot Erler amesema bado pana muda wa kuuokoa mkataba huo.Bwana Erler ameeleza kuwa mlango wa kufikia mapatano bado haujafungwa kabisa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com