1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Wito wa kuzingatia ulinzi wa wakimbizi.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuF

Mkuu wa uhamiaji wa Umoja wa Ulaya amezitaka serikali za Ulaya ziweke viwango vya hali ya juu vya kuwalinda wakimbizi.

Wito huo ni sehemu ya mpango wa kuandaa sera ya pamoja ya uhamiaji na ukimbizi kufikia mwaka 2010.

Kamishna wa sheria na mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya, Franco Frattini, ametoa mapendekezo yaliyolenga kuwepo kwa taratibu zinazowiana na pia haki na ufadhili wanaopewa wakimbizi barani Ulaya.

Mapendekezo hayo, yatakayojadiliwa na mawaziri wa sheria na mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya, yametolewa wakati ambapo kuna tofauti nyingi kuhusu jinsi ya kushughulikia wimbi la hivi karibuni la wakimbizi kutoka Afrika.