1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Wito kuwarejesha nyumbani wauguzi

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhU

Umoja wa Ulaya umeihimiza Libya kuwapeleka nyumbani wauguzi 5 wa kigeni waliopewa adhabu ya kifungo cha maisha badala ya kifo kwa mashtaka ya kuwaambukiza watoto,virusi vya UKIMWI.Baraza la Kuu la Kisheria la Libya,lilibadilisha adhabu hiyo,baada ya familia za watoto kuondosha madai yao ya kutaka adhabu ya kifo,baada ya kupatikana kwa maafikiano ya kulipwa fidia ya mamilioni ya Dola.Waziri wa masuala ya nje wa Bulgaria Ivaylo Kalfin amesifu uamuzi wa Libya,lakini alitoa wito wa kuwapeleka wafungwa hao nyumbani Bulgaria.Waziri mwenzake wa Libya Abdel-Rahman Shalgam amesema,Tripoli itafikiria kuwahamisha wafungwa hao waliozuiliwa nchini Libya tangu mwaka 1999.