1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Wabeligiji wanachagua mabaraza ya mitaa

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4y

Nchini Ubeligiji hii leo kunafanywa uchaguzi wa mabaraza ya mitaa.Uchaguzi huo ukitangulia uchaguzi wa bunge mwakani,unatazamwa kama ni mtihani kwa serikali ya waziri mkuu Guy Verhofstadt.Hasa kinachotazamwa ni vipi chama cha Vlamse Belang kinachopinga wageni,kitachomoza katika uchaguzi wa leo.Miaka sita ya nyuma,chama hicho kilijikingia theluthi moja ya kura katika mji wa bandari wa Antwerp na kuwa chama chenye usemi mkubwa wa kisiasa.