BRUSSELS : Hakuna uvumbuzi mazungumzo ya Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 15.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS : Hakuna uvumbuzi mazungumzo ya Kosovo

Duru mpya ya mazungumzo juu ya hatima ya kudumu ya jimbo la Serbia la Kosovo imemalizika bila ya kufikiwa kwa maendeleo yoyote ya maana.

Taarifa iliyotolewa na wapatanishi wa pande tatu wa Umoja wa Ulaya,Urusi na Marekani imesema maafisa wa Serbia na Kosovo wamekazania misimamo yao.Mazungumzo hayo yanazingatia mpango wa Umoja wa Mataifa ambao ungelilipatia jimbo hilo lenye watu wengi wa kabila la Waalbania uhuru.

Serbia inapinga pendekezo hilo na Urusi imesema kwamba itatumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupinga hatua yoyote ile ya kutekeleza mpango huo.

Duru ya pili ya mazungumzo hayo imepangwa kufanyika tarehe 22 mwezi wa Oktoba mjini Vienna.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com