1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: EU yataka pande hasimu nchini Ukraine kutanzua tofauti zao

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCn

Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kumalizwa kwa amani mzozo wa kisiasa huko Ukraine baada ya Rais mwenye mrengo wa kimagharibi Victor Yushchenko kutangaza kulivunja bunge, huku bunge nalo likigomea uamuzi huo.

Msemaji wa Umoja huo wa Ulaya, amesema kuwa Sekreterieti ya umoja wa Ulaya inazitaka pande zote mbili kutanzua kwa amani hali hiyo.

Rais Yushchenko amekuwa akimlaumu Waziri Mkuu Vicktor Yanukovich ambaye anaegemea upande wa Urusi kwa kujitafutia nguvu za kisiasa kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Mjini Kiev maelfu ya wafuasi wa Waziri Mkuu huyo wanaadamana na wameweka kambi katika jengo la bunge la nchi hiyo.Nao wafuasi wa Rais Yushchenko wamesema kuwa wataweka kambi jirani na hapo.

Waziri Mkuu Yanukovich alijitokeza na kuwahutubia wafuasi wake.

Rais Yushchenko ametangaza tarehe 27 mwezi ujayo kuwa tarehe ya uchaguzi mpya.Lakini wabunge wa nchi hiyo wamepinga wakisema kuwa uamuzi huo ni kama mapinduzi ya kijeshi.