1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brown atetea uamuzi wa kuwafukuza wanadiplomasia wa Urusi

17 Julai 2007

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amefanya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel akiwa katika ziara yake rasmi ya kwanza.Mkutano huo uligubikwa na mvutano wa kidiplomasia na nchi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/CB2n
Gordon Brown
Gordon BrownPicha: AP

Bwana Brown anatetea uamuzi wa serikali yake wa kuwafukuza wanadiplomasia wanne wa Urusi kutoka nchini mwake.Wanadiplomasia hao waliandamana kupinga uamuzi wa nchi ya Urusi wa kukataa kuwarejesha nyumbani mshukiwa wa mauaji ya jasusi wa zamani Alexander Litvinenko.Litvinenko jasusi wa zamani kwenye shirika la KGB la Urusi aliuawa mjini London.

Bi Merkel alisema kuwa anaunga mkono uchunguzi unaofanywa na Uingereza kuhusiana na mauaji hayo.