BRISTOL: Washukiwa ugaidi 2 wameachiliwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 21.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRISTOL: Washukiwa ugaidi 2 wameachiliwa huru

Polisi nchini Uingereza imewaachia huru watu 2 waliozuiliwa kwa kushukiwa ugaidi.Watu hao wawili walikamatwa siku ya Jumatano wakati wa msako wa madawa ya kulevya,baada ya kugunduliwa vitu ambavyo vingeweza kuhusika na harakati za kigaidi.Wakati huo huo,mahakama mjini London, imeamua kumbakisha kizuizini mshukiwa wa nne aliekamatwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi, ambapo mabomu yalishindwa kuripuka katika miji ya Glasgow na London.Idadi ya watu walioshtakiwa kupanga njama ya kutaka kusababisha miripuko,sasa ni wanne baada ya daktari Mohamed Asha kushtakiwa siku ya Alkhamisi.Mshukiwa mmoja bado anahojiwa kizuizini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com