1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BREMEN: Uchaguzi wafanywa Bremen.

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2S

Wakazi wamepiga kura zao kwenye uchaguzi wa kimkoa wa jimbo la Bremen, kaskazini mwa Ujerumani

Kura za maoni katika jimbo hilo ambalo ni dogo zaidi miongoni mwa majimbo kumi na sita ya Ujerumani, zinaonyesha meya wa sasa, Jens Böhnsen wa chama cha Social Demokratic, SPD, atahifadhi wadhifa wake wa umeya.

Chama cha SPD pamoja na chama cha kijani vinatarajiwa kupata ushindi mkubwa.

Ushindi wa SPD katika jimbo hilo la Bremen ni muhimu sana katika ngazi ya kitaifa hasa wakati huu ambapo chama hicho kimepania kuhakikisha kinadumisha umaarufu wake kwenye serikali ya mseto inayoongozwa na kansela Angela Merkel wa chama cha CDU.

Kumekuwa na tetesi huenda ushirikiano wa miaka kumi na miwili kati ya SPD na CDU ukavurugika kutokana na uhusiano uliozorota kati ya vyama hivyo viwili kuhusu masuala kama vile vita dhidi ya ugaidi, marekebisho ya utozaji ushuru na miito inayohusu mishahara ya kima cha chini.