1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRASILIA: Rais wa Brazil Lula da Silva aongoza katika matokeo ya awali

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD70

Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi. Hata hivyo amepungukiwa na idadi ndogo ya kura kumuwezesha kupata wingi wa kura ili kuzuia duru ya pili ya uchaguzi.

Huku asilimia 83 ya kura zikiwa zimehesabiwa, rais Lula da Silva amepata asilimia 49,6 ikilinganishwa na 40.7 alizopata mpinzani wake Geraldo Alckmin, gavana wa Sao Paolo.

Rais Lula anahitaji zaidi ya asilimia 50 ya kuta kushinda uchaguzi uliofanyika jana nchini Brazil. Iwapo atashindwa kufikisha idadi hiyo, atalazimika kupambana tena na mpinzani wake katika duru ya pili mnamo tarehe 29 mwezi huu.