1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiDjibouti

Boti ya wahamiaji yazama Djibouti na kuuwa watu 16

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Karibu watu 16 wamekufa maji na 28 hawajulikani waliko kufuatia ajali ya boti ya wahamiaji katika pwani ya Djibouti.

https://p.dw.com/p/4f6MK
Mili ya watu waliokufa kutokana na ajali ya boti
Mili ya watu waliokufa kutokana na ajali ya botiPicha: International Organization for Migration/AP/picture alliance

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji - IOM limesema boti iliyokuwa na wahamiaji 77 wakiwemo watoto ilizama katika pwani ya taifa hilo la eneo la pembe ya Afrika. Msemaji wa IOM Yvonne Ndege amesema tawi la shirika hilo nchini humo linashirikiana na maafisa katika juhudi za uokozi.

Balozi wa Ethiopia nchini Djibouti Berhanu Tsegaye alisema kuwa boti hiyo ilikuwa na wahamiaji wa Ethiopia kutoka Yemen na kwamba ajali hiyo ilitokea jana usiku karibu na Godoria kaskazini mwa Djibouti.

Amesema watu 33, akiwemo mwanamke mmoja wamenusurika. Boti nyingine iliyokuwa na zaidi ya watu 60 ilizama katika pwani ya Godoria mnamo Aprili 8, kwa mujibu wa IOM na ubalozi wa Ethiopia nchini DJIBOUTI.