Bonn:Bettermann achaguliwa tena kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bonn:Bettermann achaguliwa tena kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle.

Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle, ERIK BETTERMANN amechaguliwa tena kukiongoza kituo hiki cha matangazo ya kimataifa kwa kipindi kingine cha miaka sita.

Wawakilishi wa baraza la usimamizi wa shughuli za Radio wanasema mwanasiasa huyu mwenye umri wa miaka 62 ameifanya Deutsche Welle ijulikane zaidi ndani na nje ya Ujerumani tangu alipokabidhiwa kwa mara ya kwanza hatamu za uongozi mnamo mwaka 2001.

Bwana ERIK BETTERMANN amepanua matangazo kwa lugha ya kiarabu pamoja na mtandao wa Internet.Baada ya kuchaguliwa tena.

Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle ERIK BETTERMANN amesema:

„Ningependelea kuingia katika madaftari ya historia ya Deutsche-Welle ,mkitaka,kama mtu aliyetoa mchango katika kukabiliana na changamoto za utandawazi ulimwenguni.Na hayo yatawezekana tuu ikiwa sote,tutashirikiana.“

Mhula wake wa sasa unamalizika september mwakani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com