1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boateng, Hummels kukosa mchuano dhidi ya Gibraltar

8 Juni 2015

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew ameahidi kukaza kamba katika michuano ijayo dhidi ya Marekani na Gibraltar lakini anakiri kuwa hisia za msisimko huenda zinakosekana.

https://p.dw.com/p/1Fdcs
Deutschland Fußball EM-Qualifikation Jerome Boateng und Mats Hummels
Picha: picture-alliance/dpa/T. Eisenhuth

Ujerumani itashuka dimbani katika mchuano wa kirafiki dhidi ya Marekani mjini Cologne siku ya Jumatano kabla ya kupambana na Gibraltar katika mchuano wa kufuzu katika dimba la mataifa ya Ulaya - Euro 2016. Mpambano huo utachezwa mjini Faro, Ureno siku tatu baadaye.

Manuel Neuer, Thomas Mueller na Toni Kroos wameachwa nje ya kikosi lakini Patrick Herrmann wa Borussia Moenchengladbach amepewa fursa ya kucheza. Mats Hummels wa Borussia Dortmund alijiondoa jana katika timu ya taifa kutokana na maumivu ya nyonga lakini nafasi yake imejazwa na Jerome Boateng wa Bayern Munich.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu