1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blair kutangaza kuondoa askari 3000 mwaka huu kutoka Irak

21 Februari 2007

Waziri mkuu Tony Blair wa uingereza, atalihutubia Bunge alaasiri ya leo kutangaza kwamba hadi askari 3000 kati ya wote 7000 wa uingereza watarudi nyumbani gadi x-masi mwaka huu.

https://p.dw.com/p/CHJh

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair, anatarajiwa kutangaza hivi punde kurejeshwa nyumbani sehemu ya vikosi vya Uingereza viliopo nchini Irak.Hadi askari 3,000 kati ya wote 7.000 inapangwa kuwarejesha nyumbani.Kikundi cha kwanza kitakuwa cha askari 1.500 ambacho hadi x-masi mwaka huu, kiwe kimeshafunga virago.

Waziri mkuu Tony Blair anatazamiwa adhuhuri ya leo kutoa tangazo muhimu bungeni mjini London kuhusiana na uamuzi huo wa kuondoa sehemu ya vikosi vya Uingereza nchini Irak.Kusema kweli, tangu mwishoni mwa wiki tangazo hilo likisubiriwa ,kwani jumapili tu waziri mkuu Blair alizieleza shughuli zilizoitwa “Sinbad” kusini mwa Irak zilizofanikiwa.

“Opresheni tulioifanya mjini Basra sasa imekamilika.Azma yake ilikuwa kuvikabidhi vikosi vya usalama vya Irak dhamana ya safu ya mbele kabisa kusimamia salama katika mji huo.”

Alisema waziri mkuu Blair.Kwa muujibu wa labari ilizopata Idhaa ya BBC katika tangazo lake analopanga kutoa adhuhuri hii kusema pia endapo hali ya mambo itachafuka huko aweza kuchelewesha kasi ya kuondoa vikosi hivyo.Wasi wasi huo ulibainika pia katika mazungumzo yake aliofanya jumapili aliposema:

“Yafaa kuhakikisha kwamba kuna wanajeshi wa kutosha kuwasaidia wairaki pakizuka tatizo maalumu.”

Kwa jumla hatua ya uzingereza ya kuondoa sehemu ya vikosi vyake kutoka Basra,kusini mwa Irak inagongana na haipatani na mango wa Marekani wa kuongeza vikosi mjini Baghdad.

Blair anadai Basra huwezi kuulinganisha na Baghdad.

“Mjini Baghdad kuna uasi wa wasuni,kujitoa-mhanga wafuasi wa Al Kaida wanaojiripua na kuna machafuko yanayoshikamana na madhehebu ya kidini.

Hali kama hii, imepungua mno mjini Basra,kwani huko hakuna uasi wa wasuni wala tatizo la Al kaida.”

Bingwa wa kingereza wa maswali ya ulinzi, Dan Plesh, anadai kwamba nyuma ya pazia, uamuzi wa Uingereza kuhama hatua kwa hatua kutoka Irak ,hakutaipendeza Marekani:

Wengi huko anasema Plesh, watakitafsiri kitendo hicho ni kusalim amri kwa waingereza kwa wairani. Kwani, anasema, ushawishi wa Iran, kusini mwa Irak, wanamoishi washia wengi mno, ni mkubwa mno na Bush alikwisha nadi mwanzoni mwa mwaka huu, kupambana nao kijeshi .