1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blair amuunga mkono rais wa Palestina, Abbas

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CBHr

GAZA

Rais wa mamlaka ya wapalestina Mahamoud Abbas ametoa nafasi ya mwisho kwa chama cha Hamas kuwa na mazungumzo na chama cha upinzani cha Fattah katika majadiliano ya kuundwa kwa serikali ya kitaifa.

Mahamod Abbas amesema pia kuwa ataendelea na mpango wa kuitishwa kwa uchagzi mapema, kama hatakuwa na njia nyingine ya kutanzua mzozo huo.

Rais huyo wa mamlaka ya wapalestina alizungumzo saa chache baada ya vyama hivyo hasimu kufikia muafaka wa kusitisha mapigano ambayo mpaka sasa yamepelekea watu kumi kuuawa.

Leo asubuhi kulikuwa na mapigano makali karibu na makazi ya Rais wa Palestina kuwania udhibiti wa serikali.

Hapo jana Msafara wa Waziri wa mambo nje wa Palestina ulishambuliwa.

Waziri Mkuu Ismail Haniya amemlaumu Rais Mahamoud Abbas kwa kutia utambi katika mzozo huo, kufuatia wito wa kuitisha uchaguzi mapema.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Uingereza Tonny Blair amempongeza Mahampud Abbas na kuitaka kujumuiya ya kimataifa kumuunga mkono.

Akizungumza mjini Ramallah katika ukingo wa Magharibi, baada ya mkutano wake na rais huyo wa Palestina, Tonny Blair amemsifu kiongozi huyo kwa kuitisha uchaguzi mapema.

Tonny Blair amesema kuwa hata hivyo maamuzi yote wanayo wapalestina wenyewe.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Palelstina Ismail Haniya amesema kuwa serikali yake ya Hamas iko tayari kusitisha mapigano na Fattah.