BLACKSBURG:Mwanafunzi mwuuaji CHO SEUNG HUI | Habari za Ulimwengu | DW | 19.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BLACKSBURG:Mwanafunzi mwuuaji CHO SEUNG HUI

Mwanafunzi alieua watu 32 kwenye chuo kikuu cha ufundi cha Virginia,CHO SEUNG HUI alituma kifurushi cha barua, ukanda wa video na picha, kwa shirika la televisheni la Marekani NBC.

Katika barua hizo hayati mwanafunzi huyo analalamika juu ya kushinikizwa. Amesema watu walikuwa na mawezekano chungutele ya kuepuka siku ya mauaji, lakini waliamua kumwaga damu yake.

Amelalamika juu ya kusakamwa, kutiwa magonjwa akilini na kujazwa hofu moyoni.

Kijana huyo pia alieleza juu ya kuvutiwa na mauaji yaliyotokea kwenye shule ya Columbine mnamo mwaka 1999.

Shirika la NBC limesema kuwa kifurushi hicho kilitumwa karibu muda wa saa mbili baada ya kijana huyo kuwaua wanafunzi wawili. Nusu saa baadae ndipo alipowaua watu wengine 30 kabla ya kujiua .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com