1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BLACKBURG,Virginia : Muuaji wa Virginia atambulika

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9B

Mtu ambaye amewapiga risasi na kuwauwa watu 32 katika Chuo Kikuu cha Virginia kabla ya kujiuwa mwemnyewe ametambulika kuwa ni mwanafunzi wa Korea Kusini na alikuwa akiishi kwenye bweni la wanafunzi la chuo hicho.

Rais wa chuo kikuu hicho Charles Steger amewaambia waandishi wa habari kwamba Cho Seung Hui alikuwa hana mshirika katika shambulio hilo.

Wakati huo huo baadhi ya watu walionusurika na shambulio hilo pamoja na jamaa za wahanga wamekuwa wakiuliza kwa nini maafisa wameshindwa kukifunga chuo hicho baada ya kutokea kwa shambulio la kwanza la risasi.Katika shambulio la kwanza watu wawili wameuwa kwenye bweni la kulala wanafunzi, shambulio la pili ambapo wanafunzi 30 wameuwawa limekuja masaa mawili baada ya shambulio la kwanza.

Rais George W. Bush na mkewe Laura watashiriki katika ibada ya maombolezo katika Chuo Kikuu cha Virginia leo jioni.Shambulio hilo linaelezwa kuwa ni baya kabisa kuwahi kushuhudiwa tokea mauaji ya Chuo Kikuu cha Texas hapo mwaka 1966.

Polisi imesema bado haikuweza kufahamika nini dhamira ya muuaji huyo.