1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISHKEK:Bunge laidhinisha katiba mpya

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCul

Bunge la Kyrgystan limeidhinisha katiba mpya inayopunguza madaraka ya rais.

Hatua hii imevungua njia ya kumalizika kwa mzozo wa kisiasa katika nchi hiyo ya Asia ya Kati ambako kumekuwa na ghasia tangu jumanne iliyopita.

Wafuasi wa upinzani na wale wa rais Kurmanbek Bakiyev wamekuwa wakipambana kwenye barabara za mji huo kuhusu suala hilo la katiba mpya.

Katiba hiyo imeidhinishwa baada ya bunge kupiga kura ambapo wabunge 67 kati ya 75 waliunga mkono.

Rais Bakiyev anabidi kutia saini katiba hiyo.