1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BISHKEK: Waandamanaji wamiminika mji mkuu wa Kyrgyzstan

Maandamano makubwa yanafanywa leo hii nchini Kyrgyzstan huku viongozi wa upinzani wakimtaka rais Kurmanbek Bakiyev aondoke madarakani.Maelfu ya polisi wametawanywa katika mji mkuu Bishkek ambako waandamanaji wanaendelea kumiminika.Hapo awali rais Bakiyev aliukataa wito wa upinzani wa kumtaka afanye mageuzi ya katiba moja kwa moja ili kupunguza mamlaka yake.Bakiyev vile vile ametoa wito wa kusitisha maandamano.Rais Bakiyev alishika madaraka baada ya kupata ushindi mkubwa mwaka jana,lakini wakosoaji wanaituhumu serikali yake kuwa inashindwa kukomesha ulajirushwa uliozagaa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com